Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za posta kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano: Profesa Tibaijuka

Huduma za posta kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano: Profesa Tibaijuka

Kongamano la 25 la Shirika la kimataifa la posta, UPU limefanyika Doha, Qatar kuanzia tarehe 7-11 Oktoba mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine nchi 192 wanachama wa shirika hilo waliangalia nafasi ya huduma za posta duniani kwenye maendeleo ya sasa ya teknolojia ya mawasiliano na kumulikia hasa anwani za makazi na utashi wa kisiasa wa kutekeleza mpango huo. Miongoni mwa washiriki ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni Balozi maalum wa anwani za makazi wa UPU na katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa huduma za posta na alianza na anwani ya posta ya makazi alipohojiwa na Assumpta Massoi.

(MAHOJIANO NA ANN TIBAIJUKA)