Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu la UM laongeza muda wa kuhudumu wa tume ya uchunguzi nchini Syria

Baraza la haki za binadamu la UM laongeza muda wa kuhudumu wa tume ya uchunguzi nchini Syria

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa hii leo limepitisha azimio sita ambapo limeongeza muda wa kuhudumu kwa tume ya kimataifa ya uchunguzi nchini Syria na pia kuongeza muda wa kuhudumu kwa mtaalamu huru nchini Sudan kwa mwaka mmoja zaidi. Azimio la Syria lilipitishwa kwa kura 41 ambapo mataifa ya China, Cuba na Urusi yalipinga.

Baraza hilo hilo pia lilipitisha azimio la haki za binadamu nchini Mali, azimio la msaada ya kiufungu nchini Sudan Kusini hasa kweye nyanja ya haki za binadamu na azimio kuhusu haki za watu wazee na wale wa kutoka jamii za kiasili. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)