Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya amani yanafaa kufanywa bila vitisho:UM

Mazungumzo ya amani yanafaa kufanywa bila vitisho:UM

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuendeleza utaratibu wa kimataifa wa demokrasia na usawa, Alfred de Zayas, ametoa wito kwa mataifa na mashirika ya umma kujitahidi katika kumaliza mizozo kwa njia ya amani, kuvumilia katika desturi ya kufanya mazungumzo, na kukataa dhana ya vita.

Bwana de Zayas amesema hayo katika ujumbe wake kwenye siku ya kimataifa ya amani, ambayo huadhimishwa kila tarehe 21 Septemba.

Amesema kila mazunguzmo ya amani yanapokwama na mataifa kushikilia misimamo mikali, ni wakati wa kuacha misimamo hiyo kama njia ya kuafikiana. Amesema kila mmoja anafaa kujiondolea desturi ya uwindaji wa wengine, ubaguzi, pamoja na kujigamba. Ameongeza kuwa amani ni haki inayowezesha vitu kufanyika, na ambayo inahitajika ili kufurahia haki za umma, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni.