Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha kuachiliwa kwa walofungwa kwa kuwa na dhana tofauti Myanmar

UM wakaribisha kuachiliwa kwa walofungwa kwa kuwa na dhana tofauti Myanmar

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadam nchini Myanmar, Tomás Ojea Quintana, amekaribisha hatua ya msamaha wa rais wa nchi hiyo ambapo watu kadhaa walofungwa kwa kuwa na dhana tofauti wameachiliwa, na kutoa wito waachiliwe wafungwa wote kama hao mara moja, na bila masharti yoyote.

Amesema hatua za ujasiri zinahitajika sasa ili kuepukana na sifa za zamani, na kuhakikisha kuwa hakuna wafungwa wowote wa dhana wameachwa nyuma.

Amesema hili linahitaji serikali kushirikiana na wadau wengine, kama vile mashirika ya kisiasa na ya umma, ili kuweka wazi ni wafungwa wangapi wa dhana bado wapo, na kuweka mfumo unaoruhusu uhuru wa kutembelea magereza.

Miongoni mwa wale walioachiliwa ni U Khaymar Sara, mfuasi wa dini ya Buddha ambaye alikuwa kizuizini tangu maandamano ya mwezi Septemba 2007, na ambaye alitembelewa na mtaalam huyo maalum alipozuru Myanmar mwezi Agosti. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)