Shule kufunguliwa mwezi huu nchini Syria: UNICEF

14 Septemba 2012

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa shule  nchini Syria zitaanza muhula mpya tarehe 16 mwezi huu. Wizara ya elimu nchini Syria inasema kuwa shule 272 kati ya shule 22,000 zimeharibiwa huku shule 801 zikiwa ndizo makao kwa watu waliohama makwao.

UNICEF imesaidia katika ukarabati wa shule 67 huku serikali ikihamisha wale waliopiga kambi shuleni kwenda kwa majengo ya serikali. UNICEF inasema kuwa ni jambo muhimu ikiwa watoto wanaweza kurudi shuleni na pia kuwapa fursa ya kukutana na wenzao.

Watoto walioandikishwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR hawatalipishwa karo. Nchini Lebanon watoto 32,000 kutoka Syria wanatarajiwa kujiunga na shule. Marxie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter