Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM lataka kukakimilika kwa amani kipindi cha mpito nchini Somalia

Baraza la Usalama la UM lataka kukakimilika kwa amani kipindi cha mpito nchini Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha kupitishwa kwa katiba mpya nchini Somalia, kuchaguliwa kwa bunge pamoja na kuteuliwa kwa spika ambapo limetoa wito kwa pande zote kushirikiana kuhakikisha kuwa kipindi cha mpito kumekamilika kwa njia ya amani.

Professor Mohammed Osman Jawari alichaguliwa kama spika kwa bunge jipya uchaguzi ambao uliweka msingi wa kuteuliwa kwa manaibu wawili wa Spika shughuli ambayo itafuatiwa na kuchaguliwa kwa rais wa taifa hilo la pembe ya Afrika. Baada ya miaka mingi ya vita Somalia imekuwa kwenye mchakato wa amani huku serikali ya mpito ikitekeleza kile kijulikanacho kama barabara ya amani ya kumaliza kipindi cha mpito. Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamelitaka bunge jipya kutoa huduma zake kwa njia iliyo huru na yenye uwazi.