Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande hasimu nchini Syria zimeshindwa kuwalinda Raia:Amos

Pande hasimu nchini Syria zimeshindwa kuwalinda Raia:Amos

Majeshi ya serikali na wapiganaji wa upinzani nchini Syria wameshindwa kutekeleza sheria za kimataifa za kuwalinda raia.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Jumatano baada ya kukamilisha ziara yake Syria Bi Amos amesema watu milioni 2.5 wanahitaji msaada wa haraka. Ameongeza kuwa huduma za afya, malazi, chakula, maji na safi ni miongoni ya mahitaji hayo ya haraka. Bi Amos ambaye alikuwa Syria wiki iliyopita amesema hali imekuwa mbaya zaidi tangu alipozuru nchi hiyo mwezi Machi.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)

"Pia nitatiwa hofu kwamba pande husika katika vita zimeshindwa kuwalindwa kutekeleza sheria za kimataifa ambazo zinaweka bayana taratibui za kuwalinda raia.Mgogoro huu umekuwa wa kikatili na wenye ghasia kubwa. Wote tumeona picha za kutisha na kuusikitisha kwenye runinga na ni za wanawake wa kawaida, wanaume na watoto ambao wamejikuta katikatio ya zahma. Narejea wito wangu kwa wote ambao wanshiriki vita kuheshim raia na kutimiza sheria za kimataifa za kibinadamu.”

Bi Amos amesema ingawa Umoja wa Mataifa na washirika wake wanawafikia watu Syria,ufadhili wa fedha na fursa ya kuingia kwenye maeneo yenye mapigano makali imesalia kuwa changamoto.