Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa OCHA yuko nchini Syria Kuchagiza Jitihada za Kuwafikishia Waathirika Misaada

Mkuu wa OCHA yuko nchini Syria Kuchagiza Jitihada za Kuwafikishia Waathirika Misaada

Mratibu Mkuu wa Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Bi Valerie Amos, amewasili nchini Syria kwenye ziara ya siku tatu, ili kukagua hali ilivyo na jinsi ya kuwasaidia watu walioathiriwa na machafuko. Mjini Damascus, Bi Amos amepanga kufanya mazungumzo na maafisa wa serikali na wadau katika utoaji wa huduma za kibinadamu, pamoja na familia zilizoathiriwa na mgogoro wa Syria. Kwa mujibu wa msemaji wa OCHA, Jens Laerke, Bi Amos yupo Syria kuelezea kusikitishwa kwake na hali ya kibinadamu iliyopo.

Bwana Laerke ameongeza kuwa Bi Amos atakagua hali halisi ilivyo, na mazungumzo yake na serikali na wadau katika huduma za kibinadamu yatalenga jinsi ya kuongeza jitihada za kuwasaidia watu walioathirika na mzozo wa Syria.

(SAUTI YA JENS LAERKE)