Tunajitahidi kwa kila njia kuwekeza kwa wanawake:Ban

13 Agosti 2012

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujuma wanajitahidi kwa kila njia kuwekeza kwa wanawake ili wafikie malengo ya kuchagiza maendeleo na kuipeleka dunia katika mstakhbali bora.

Ban ameyasema hayo mjini Seuol Korea Jumatatu kwenye kongamano la kwanza la kimataifa la shirikiano wa wasichana. Ban amesema siku zote ubaguzi wa kijinsia ni kikwazo cha kupiga hatua, na usawa unawezesha kufikia masala mengi. Ameongeza kuwa kutokuwepo kwa uwakilishi wa wanawake na kwawezesha wanawake kunaathiri haki binafsi za wanawake hao na hivyo kurudisha nyuma taifa zima.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa kuwasaidia wanawake ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015. Wanawake wengi wanafanya kazi sana na kulipwa ujira mdogo kuliko wanaume. Wanawake wanazalisha asilimia 80 ya chakula chote Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara lakini nyumba zao ndio masikini zaidi na wanamiliki mali chachw sana kliko wanaume.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter