Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angola yaadhimisha mwaka mmoja bila Ugonjwa wa Polio

Angola yaadhimisha mwaka mmoja bila Ugonjwa wa Polio

Angola leo imeadhimisha mwaka mmoja wa kutokuwa na tukio lolote la ugonjwa wa polia na hivyo kuongeza msukumo kwenye jihada za kimataifa za kukabiliana na ugonjwa huo duniani kote.

Kiwango cha ugonjwa huo katika mwaka 2010 kilipungua na kufikia wagonjwa 33 na hali ya kuimarika zaidi ilishuhudiwa mwaka uliofuata 2011 kukiwa na wagonjwa wa tatu tu. Na ndani ya mwaka 2012 hakuna mgonjwa yoyote aliyeripotiwa.

Hadi kufikia mwezi July mwaka jana vipimo vya maabara vilionyesha kupatikana kwa mtoto mmoja aliyekuwa naumri wa miezi 14 ambaye alikumbwa na ugonjwa huo katika jimbo la Uige lililoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeelezea hali hiyo kuwa ni mafanikio makubwa ambayo ni matokeo ya kampeni kubwa ya utoaji chanjo iliyoendeshwa katika taifa hilo.