Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuanza kuchunguza tuhuma za ubakaji wa halaiki DRC

UM kuanza kuchunguza tuhuma za ubakaji wa halaiki DRC

Umoja wa Mataifa umeanzisha shabaya ya kuendesha uchunguzi kuhusiana na taarifa za kufanyika kwa ubakaji wa halaiki unaodaiwa kufanywa katika eneo la mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Tayari timu ya wachunguzi imeandaliwa ambayo itatumwa katika eneo la Nyakiele lililoko Kivu Kusin ambako ubakaji huo unadaiwa kufanywa.  Ripoti za hivi karibu zinasema kuwa shirika la Médecins Sans Frontières, limetoa huduma ya matibabu kwa waathirika zaidi ya 100 ambao walikumbwa na vitendo hivyo.

 Wengi wa waathirika hao wanakabiliwa na matatizo ya kiafya lakini wengine wamejikuta wakiishi kwenye hali ya hofu na mashaka.