ILO yazingatia mienendo inayoweza kusaidia kubadili hali ya ajira kwa vijana

10 Agosti 2012

Shirika la Ajira Duniani, ILO, limesema kuendeleza ajira kwa vijana limekuwa suala la kipaumbele kwa serikali nyingi, wakati vijana milioni 75 kote ulimwenguni hawana ajira.

Hata hivyo, shirika la ILO limeonya kuhusu kizazi cha vijana chenye vidonda vinanyotokana na ukosefu wa ajira, kukaa tu bila cha kufanya, ajira zenye hatari pamoja na umaskini ulokolea katika mataifa yanayoendelea.

Shirika la ILO limesema siku ya kimataifa ya vijana inayoadhimishwa kila Agosti 12 ina lengo la kuwafanya watu wazingatie masuala yanayowaathiri vijana kote ulimwenguni, na pia ni fursa ya kuangazia baadhi ya sera na mienendo inayoweza kusaidia kukabiliana na tatizo za ajira kwa vijana. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter