Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufanya kazi na vijana na kwa ajili yao ni mojawepo ya mambo muhumu zaidi kwangu:Ban

Kufanya kazi na vijana na kwa ajili yao ni mojawepo ya mambo muhumu zaidi kwangu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa kizazi cha sasa cha vijana, ambacho ni chenye idadi kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni, wengi wao wakipatikana katika nchi zinazoendelea, kina uwezo mkubwa zaidi wa kuendeleza jamii nzima ya binadamu. Bwana Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya vijana, ambayo huadhimishwa kila Agosti 12.

Bwana Ban amesema, licha ya uwezo huo wa vijana, wengi wao, wakiwemo wale wenye kisomo cha juu, bado wanakumbwa na matatizo ya mishahara midogo, ajira zisizotoa matumaini na ukosefu wa ajira wa kupindukia.

Amesema mdororo wa uchumi wa duniani umeathiri zaidi vijana, na wengi wao wamevunjwa moyo na kutokuwepo usawa kunakoongezeka. Amesema mojawepo ya mambo anayoyapa kipaumbele ni kufanya kazi na vijana, na kwa ajili yao.