Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyombo vya Habari vya Kijamii vinatoa fursa kwa jamii ya Watu wa Asili:ILO

Vyombo vya Habari vya Kijamii vinatoa fursa kwa jamii ya Watu wa Asili:ILO

Katika muktadha huo wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wa kiasili leo, Shirika la Kimataifa la kazi duniani, ILO, limesema vyombo vya habari vya kijamii vinachangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza haki za watu wa kiasili.

Shirika la ILO limesema hili linatokana na kwamba, takriban nusu ya idadi ya watu wa kiasili kote ulimwenguni wanaishi mijini, ambako kujiunga kwa mitandao ya habari ya elektroniki ni rahisi.

Kwa sababu ya mtandao wa internet, inachukua sekunde chache tu kwa habari kuwahusu watu wa kiasili kusambaa kutoka sehemu moja ya dunia hadi nyingine. Jason Nyakundi na taarifa kamili

(SAUTI YA JASON)

Nao wananchi wa Afrika ya Mashariki wanasemaji kuhusu siku hii ya watu wa asili na haki zao?

(MAONI YA AFRIKA YA MASHARIKI)