Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yalaani mauaji ya mfanyakazi wake Kordofan Kusini

WFP yalaani mauaji ya mfanyakazi wake Kordofan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP Jmapili limelaani vikali mauaji ya mmoja wa madereva wake katika shambulio kwenye jimbo la Sudan la Kordofan Kusini ambako machafuko yanaendelea kwa kikwazo kwa juhudi za kufikisha misaada za shirika hilo.

Kwa mujibu wa WFP Jamal Al Fadil Farag Allah mwenye umri wa miaka 56 ambaye ni raia wa Sudan aliuawa kwa shambulio la silaha Jumamosi karibu na eneo la Hilat Yatu kilometa 80 Kaskazini mwa Kaduggli mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kusini.

Jamal ambaye amekuwa akifanya kazi na WFP tangu mwaka 2005 ameacha mke na watoto watano. Na mauati yalimkuta alipokuwa awakimwendesha mfanyakazi mwenzake Saad Yousif gari lake liliposhambuliwa na watu wawili wasiojulikana. Saad alinusurika na hivi sasa anapokea matibabu. Sdan inasalia kwa moja ya maeneo yanayotoa changamoto kbwa kwa operesheni za misaada za WFP.