Masuala ya Syria na Mali yataendelea kutawala Baraza la Usalama mwezi Agosti

1 Agosti 2012

Ufaransa inaanza mzunguko wa Urais wa Baraza la Usalama mwezi huu wa Agosti na balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa anatumai kwamba kutakuwa na muafaka wa kimataifa kuhusu kuchukua hatua dhidi ya Syria.

Balozi Gérard Araud anasema ni bahati mbaya kwamba wajumbe hawajapata suluhu ya mgogoro wa Syria ambao umeshika kasi wiki za karibuni.

Balozi huyo pia amesema anataka kuona hatua ikichukuliwa dhidi ya Mali ambako mapinduzi ya kijeshi na machafuko Kaskazini mwa nchi yamewatawanya watu zaidi ya 40,000 ndani na nje ya nchi. Balozi Arad amesema mashambulizi yanayoendelea mjini Aleppo yanafanya kuwa vigumu kulifumbia macho tatizo la Syria.

(SAUTI YA GERARD ARAUD)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud