Mkutano wa CITES Kukabiliana na Biashara Haramu ya Pembe za Tembo na Vifaru

25 Julai 2012

Watu 350 kutoka kote ulimwenguni wanakusanyika mjini Geneva wiki hii kwa mkutano wa 62 wa kamati maalum kuhusu mkataba wa biashara ya kimataifa katika viumbe walio katika hatari ya kuangamizwa kabisa, CITES. Mkutano huo utaangazia jinsi ya kukabiliana na biashara haramu ya pembe za ndovu na vifaru, pamoja.

Pamoja na hayo, mkutano huo pia utajadili kuhusu nyoka wa bara Asia, simba marara, chui, kasuku, pamoja na kobe na vyura wa Madagascar, na aina vyingine za wanyama na mimea. Kamati hiyo inatarajia kuweka mbinu mwafaka za kudhibiti kikamilifu biashara katika wanyama wa pori na mimea kati ya mwaka 2013 na 2016.

Itaangazia ni nini hasa kinachochagiza biashara ya pembe ya vifaru ambayo sasa imepanda sana. Mataifa ambayo tangu jadi hununua pembe hasa ni UChina, Taiwan (Province of China), Japan, Jamhuri ya na Viet Nam, ambayo yote yamepiga marufuku biashara hiyo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter