Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaomba Juhudi Zaidi Zifanywe Kukabiliana na Ugonjwa wa Hepatitis

WHO yaomba Juhudi Zaidi Zifanywe Kukabiliana na Ugonjwa wa Hepatitis

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa wito kwa serikali kote duniani kuimarisha juhudi za kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa Hepatitis, ambao huathiri ini na unasemekana kuwaua watu milioni moja kila mwaka. Ujumbe huu wa WHO umetolewa kabla ya Siku ya Hepatitis Duniani, ambayo huadhimishwa kila Julai 28.

Takriban watu nusu bilioni huumwa mara kwa mara, kutokana na maambukizi ya vya Hepatitis, ambavyo usababisha asilimia themanini ya saratani ya ini. Dr. Sylive Briand kutoka idara ya maradhi ya kuambukiza ya Shirika la Afya Duniani, amesema watu wengi zaidi walioambukizwa Hepatitis hawajui, hawajapimwa na hawajapata matibabu. Amesema hatua ya kwanza ya kuudhibiti ugonjwa huo na kuokoa maelfu ya maisha, inawezekana kufikiwa tu kwa kufahamu aina mbali mbali za Hepatitis, kuzuia maambukizi, pamoja na kuutibu.  Alice Kariuki ana maelezo zaidi.

(SAUTI YA  ALICE KARIUKI)