Skip to main content

UM wazindua Tovuti Mpya kwa ajili ya Watoto kwenye Maeneo ya Vita

UM wazindua Tovuti Mpya kwa ajili ya Watoto kwenye Maeneo ya Vita

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye maeneo yaloathirika na vita, Radhika Coomeraswamy, leo amezindua tovuti mpya, ambayo itasheheni habari na maktaba ya maelezo muhimu kwa ajili ya wale wanaotaka kuyapata.

Tovuti hiyo http://childrenandarmedconflict.un.org itakuwa na maelezo na taarifa muhimu zinazotolewa na idara hiyo ya Umoja wa Mataifa, na kuonyesha picha kutoka maeneo ya huduma zake.

Itaambatanisha pia tovuti muhimu za mitandao ya vyombo vya habari ya kijamii, zikiwemo Facebook, Twitter, Tumblr, Youtube, Flickr, na mingine itakayowezesha kubadilishana habari, maelezo, video, na mengineyo.

Bi Coomeraswamy amesema kuwa, kupitia tovuti hii sasa, yeye na wafannyakazi wengine kwenye idara hiyo wataweza kutoa habari mara tu zinapotokea, hata wakiwa kwenye maeneo ya kazi nje ya afisi zao.