Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Wenye Ulemavu Wako kwenye Hatari ya Kudhulumiwa

Watoto Wenye Ulemavu Wako kwenye Hatari ya Kudhulumiwa

Watoto walio na ulemavu wako kwenye hatari ya kudhulumiwa mara nne zaidi kuliko wale wasio na ulemavu. Hii ni kwa mujibu wa utafiti kutoka kwa shirika la afya duniani WHO. Ripoti hiyo inasema kuwa watoto walio na ulemavu unaohusu matatizo ya kiakili na ulemavu wa viungo vya mwili wako kwenye hatari ya kudhulumiwa kimapenzi ikilinganishwa na wasio na ulemavu.

Utafiti huo uliendeshwa miongoni mwa watoto 18,374 walio na ulemavu kwenye mataifa yenye kipato cha juu yakiwemo Finland, Ufaransa , Israel, Uhispania , Sweden, Uingereza na Marekani. Dr Tom Shakespeare kutoka WHO anasema kuwa takwimu kutoka nchi zenye kipato cha wastani na cha chini hazikujumuishwa hata kama ishara ni kwamba dhuluma kwa watoto walio na ulemavu kwenye nchi hizi ni za viwango vya juu.

(SAUTI YA DR. TOM SHAKESPEARE)