Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuongeza Uzalishaji na Mfumo Endelevu Kutaimarisha Usalama wa Chakula:FAO

Kuongeza Uzalishaji na Mfumo Endelevu Kutaimarisha Usalama wa Chakula:FAO

Huku masoko ya bidhaa za kilimo duniani yakiwa yametulia sasa, baada ya viwango vya juu zaidi vya bei mwaka uliopita, bei za bidhaa za chakula zinatarajiwa kusalia juu kwa muongo mmoja ujao. Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, hali hii inasababishwa na kutopungua kuhitajika kwa bidhaa hizo, huku uzalishaji ukiendelea kupungua kote duniani.

Ripoti hiyo inasema kuwa, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu, vipato kupanda kwa jumla, na watu kuhamia mijini, kubadilisha kwa aina za vyakula katika mataifa yanayoendelea na kuongezeka kwa mahitaji ya bayo-nishati kunaongeza mashinikizo ya mahitaji ya chakula.

Wakati huohuo, ripoti inasema, uzalishaji wa kilimo katika nchi zenye umaarufu wa kijadi wa kuzalisha bidhaa hizo kwa ajili ya kuuza nje, umepungua kwa ajili ya bei kupanda katika mwongo mmoja uliopita. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Akizungumza wakati wa kuzindua ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jose Graziano da Silva amesema, suala la usalama wa chakula linatia shaka sasa, na hata kwa siku zijazo.

(SAUTI YA JOSE GRAZIANO DA SILVA)