Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yataka kuongezwa kwa elimu ya ujuzi kukabili changamoto za ongezeko la watu duniani

ILO yataka kuongezwa kwa elimu ya ujuzi kukabili changamoto za ongezeko la watu duniani

Shirika la kazi ulimwenguni ILO limeonya juu ya kile ilichokiita ongezeko kubwa la watu ambalo matokeo yake yanadhihiri kwenye vita vya kuwania ubunifu na ukuzaji vipaji.

Kwa mujibu wa ILO kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu duniani kunasukuma pia mbio za kuwania nafasi muhimu jambo ambalo limesisitiza kuwa linaacha kitisho juu ya mustakabala wa hali ya uchumi ambao katika kipindi cha miaka ya nyuma ulikumbwa na hali ya mkwamo. Hata hivyo shirika hilo ambalo limezitizama nchi katika mazingira tofauti linahimiza haja ya kuongeza kiwango cha ujuzi hasa kwa vijana ili kuzikabili changamoto zinazojili kila wakati.

ILo inasema kuwa inakadiria kuona ongezeko la idadi ya watu likiongezeka huku kiwango cha watu kuishi hasa katika nchi zilizoendelea kikizidi umri wa miaka 60, na kiwango hicho kinatazamia kudumu hata kufikia mwaka 2050