Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumeokoa maisha kutokana na njaa Somalia:UNHCR

Tumeokoa maisha kutokana na njaa Somalia:UNHCR

Mwaka mmoja baada ya janga la njaa kuanza nchini Somalia, kijana mmoja, Aden Yusef Kabey, anaweza kucheka akikumbuka uchungu aliopitia, alipokonda kupindukia, akawa hawezi kutembea, kula wala kulala. Sasa anaweza kufanya hivyo, baada ya afya yake kurejea.

Mwaka mmoja uliopita, Kabey alilala kwenye kijinyumba cha babake, akiwa amefunikwa kiraga tu. Alikuwa amewasili kutoka Ethiopia, kupitia Baidoa, akiwa na utapia mlo. Mara tu baada ya kuwasili, alipata ugonjwa wa surua, na akawa hawezi kula wala kulala.

Afya yake ilipodhoofika hata zaidi, babake alimkuta mtu wa mkokoteni wa punda na kumchukua kwenye kituo cha kutoa msaada cha Shirika la Kuhudumia Wakmbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Baada ya mwezi mmoja, maisha yake yalikuwa hayapo tena hatarini.

Jason Nyakundi anasimulia jinsi kisa cha Kabey kinavyoashiria umuhimu wa msaada uliotolewa na UNHCR katika kipindi cha mwaka mmoja, na kilichoigwa kutokana na hilo.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)