Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ayasifu Mashirika ya Umma kwa Kuongoza Juhudi za Kuondoa Hukumu ya Kifo

Ban ayasifu Mashirika ya Umma kwa Kuongoza Juhudi za Kuondoa Hukumu ya Kifo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameyasifu mashirika ya umma kwa kuwa mstari wa mbele katika juhudi za kutokomeza hukumu ya kifo. Bwana Ban amesema, haki ya kuishi ndio muhimu zaidi katika haki zote za binadam, na kwamba ni msingi wa sheria ya kimataifa ya haki za binadam. Ameongeza kuwa mwanadamu mmoja kukatiza maisha ya mwingine ni tendo la kikatili, na lisiloweza kurekebishwa, hata kama linaungwa mkono na utekelezaji wa sheria.

Amesema, pale hukumu ya kifo inapoendelea kutekelezwa, hali ya watu wanaosubiri kuuawa huwa ni ya kutisha na ya kuchangia kuteseka kwa hali ya juu, na kwamba inajulikana wazi kuwa watu wasio na hatia bado wanauawa. Mnamo mwaka 2007, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilichukuwa hatua muhimu ya kupiga marufuku hukumu ya kifo na kulinda haki za binadam pale lilipounga mkono kusitishwa kwa utekelezaji wa hukumu ya kifo kote ulimwenguni.