Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi, ukiwemo wa rangi ni lazima ukabiliwe kwa nyanja zote:UM

Ubaguzi, ukiwemo wa rangi ni lazima ukabiliwe kwa nyanja zote:UM

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki za watu wa kigeni na aina zingine za ubaguzi, ametoa wito kwa mataifa kote ulimweguni kuzingatia kwa karibu sana ishara za mwanzo za ubaguzi wa rangi, ambao hatimaye huenda ukasababisha mizozo na ukiukaji mbaya wa haki za binadamu.

Mtaalam huyo, Mutuma Ruteere, ametoa mifano ya kuibuka kwa vyama vya kisiasa na makundi mengine yenye mrengo mkali, pamoja na suala la ubaguzi wa rangi katika muktadha wa kinyang’anyiro cha kombe la UROPA. Bwana Ruteere ameliambia Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva kuwa, makundi haya yanatoa tishio kubwa hata zaidi hasa katika mazingira ya sasa ya mdororo wa uchumi.

Amesema katika muktadha huo, watu wa rangi tofauti au wageni hulengwa kama sababu ya kutokuwepo nafasi za ajira na kuongezeka deni la kitaifa. Ameongeza kuwa ubaguzi wa rangi na vitendo vya chuki za kirangi vinaendelea kufanyika dhidi ya watu wenye asili ya kiafrika na watu wengine wenye jamii ndogo kama Waroma, wanafunzi wa kigeni, Wayahudi, Waislamu na wahamiaji.

(SAUTI YA RUTEERE)