Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM Waungana na Sanaa ya Fasheni Kukabili njaa

UM Waungana na Sanaa ya Fasheni Kukabili njaa

Umoja wa Mataifa leo imetangaza kuanzisha mashirikiano ya karibu na waendeshaji wa sanaa za fasheni ili kukabiliana na tatizo la umaskini na kutoa msaada wa chakula kwa mamilioni ya wanawake na watoto wanaotabika duniani kote.

Mashirikiano hayo yanayojulikana kama fasheni kwa maendeleo F4D, yanania ya kuongeza msukumo kwenye mpango wa maendeleo ya mellenia ya Umoja wa mataifa ambayo ukomo wake unafikia mwaka 2015.

Hata hivyo mradi huo ulizinduliwa mnamo mwaka 1996 na mwanamitindo wa kimataifa Bibi Russel akipata uungwaji mkono toka Umoja kupitia shirika lake la UNESCO ukiwa na lengo la kuwaunga mkono wanawake katika nchi zinazoendelea kupata fursa bora za kiuchumi.

Kuanzishwa kwa mashirikiano hayo, kunatazamiwa pia kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa kiwango cha kati kuibuka na kupewa nafasi ya kupepeea kwenye duru za kimataifa na kuongeza kipato kwa jamii zao.