Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupambana na Ugaidi inahitaji zaidi ya Mtazamo wa Jadi wa Usalama:Ban

Kupambana na Ugaidi inahitaji zaidi ya Mtazamo wa Jadi wa Usalama:Ban

 

Inahitaji zaidi ya mtazamo wa jadi wa usalama kupambana na tatizo la ugaidi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo kwenye kongamano maalumu linalozungumzia elewa na njia za kukabili ugaidi.

Ban amesema dunia lazima ishirikiane kuzima moto wa chuki na kutovumiliana ambao ndio chachu ya kuzalisha ghasia za kigaidi. Ameongeza kuwa kutokuwepo na amani na maelewano na mazingira ya kutovumiliana miongoni mwa watu ni suala lisilo na nafasi hasa katika dunia ya sasa ya utandawazi. Amesema mambo haya yanakiuka misingi na maadili ya mikataba ya Umoja wa Mataifa. Na ndio maana amesema mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na ugaidi unasisitiza kuwepo mazungumzo na maelewano miongoni mwa jamii. Kongamano hilo limeanza Jumatano na litakamilika June 29.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)