Kuwepo ajira kwa vijana ndiyo itakuwa ajenda kuu ya vijana kwenye mkutano wa Rio+20

18 Juni 2012

Huku nusu ya watu wote duniani wakiwa chini ya umri wa maiaka 25 na hali mbaya ya uchumi ikiendelea, kuwepo kwa ajira za kisasa ili kupunguza athari za shughuli za uchumi kwa mazingira ni kati ya masuala yatakayopewa kipaumbele na vijana ambao watahudhuria mkutano kuhusu

maendeleo endelevu wa Rio+20.

Kwenye mkutano uliondaliwa na shirika la mazingira la Umoja waMataifa UNEP waakilishi kwa seriakli , maafisa wa Umoja wa Mataifa na vijana walijadili changamoto

zonazowakumba vijana na kinaachohitajika kufanywa ili vijana waweze kupata ajira.

Kati ya masuala makuu yaliyojadiliwa ni pamoja na haja ya kuwapaq vijana mafunzo kwenye shughuli zisizoathiri mazingira akiiongeza kuwa kuna pengo kubwa kati ya walio na ujuzi wa kazi na kazi zinazopatikana.