Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 800,000 walazimika kuvuka mipaka 2011:UNHCR

Wakimbizi 800,000 walazimika kuvuka mipaka 2011:UNHCR

Ripoti mpya ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, inasema mwaka wa 2011 uliweka rekodi kwa kushuhudia idadi ya wakimbizi 800,000, ambayo ndio idadi kubwa zaidi ya watu kuwahi kuvuka mipaka kama wakimbizi,tangu mwaka 2000.

Ripoti hiyo ambayo imetolewa leo iitwayo 2011 Global Trends, inaonyesha kwa mara ya kwanza kiwango cha ukimbizi uliotokana na mizozo ya kibinadamu iliyoanzia Ivory Coast mwishoni mwa mwaka 2010, na kufuatiwa na mingine Libya, Somalia, Sudan na kwingineko. Jumla ya watu milioni 4.3 walilazimika kuhama makwao upya, wakiwemo 800, 000 waliovuka mipaka na kuwa wakimbizi katika nchi nyingine. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)