Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kaya 26,000 kunufaika na kilimo cha miti Liberia

Kaya 26,000 kunufaika na kilimo cha miti Liberia

Serikali ya Liberia imepokea kiasi cha dola za kimarekani milioni 15 kwa ajili ya kuboresha mifumo yake ya fedha na maeneo mengine ikiwemo teknolojia na upanuzi wa masoko ya uhakiki ili kuwasaidia jamii ya wakulima wadogo wadogo walioko nchini humo.

Kiasi hicho cha fedha ambacho ni mkopo toka benki ya dunia kimewalenga kuwanufaisha wakulima hao kupitia uanzishwaji wa miradi ya muda mrefu.

Mpango huo ambao unamulika zaidi sekta ya uzalishaji mazao ya miti unatazamiwa kudumu kwa kipindi cha miaka mine ukitekelezwa katika maeneo kadhaa.

Mradi huo umelenga kunufaisha jumla ya mazao ya miti yapatayo 4,900 na hivyo kuzifaidisha jumla za kaya zinazofikia 26,000 .