Annan Atumai Suluhu ya Kidemokrasia nchini Syria

30 Mei 2012

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu nchini Syria Kofi Annan amesema ni muhimu kutafuta suluhu ya kidemokrasia ambayo itasaidia kuwa na kipindi cha mpito cha kidemokrasia nchini Syria na kupata njia ya kumaliza mauaji haraka iwezekanavyo.

Annan ameyasema hayo mjini Amman Jumatano alipowasili Jordan na kuongea na waandishi wa habari, baada ya mazungumzo yake na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kuhusu mgogoro unaoendelea Syria na athari zake katika kanda nzima. Ameongeza kuwa mgogoro wa Syria ni suala gumu na la muhimu sana katika nchi jirani za kanda ya Mashariki ya Kati na dunia nzima kwa ujumla hivyo kupatikana suluhu ni lazima. Ahmed Fawzi ni msemaji wa Kofi Annan.

(SAUTI YA AHMED FAWZI)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter