Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua mpango wa kutafuta maji yaliyo chini ya ardhi katika pembe ya Afrika

UNESCO yazindua mpango wa kutafuta maji yaliyo chini ya ardhi katika pembe ya Afrika

 

Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataiafa hii leo limezindua mpango ambao una lengo la kumaliza athari zinazotokana na ukame kwenye eneo la pembe ya Afrika kupitia miradi ambayo itahakikisha upatikanaji wa maji safi yaliyo chini ya ardhi kwa watu wa eneo hilo.

Mpango huu umeanzishwa kufuatia kuwepo tatizo la ukame na ukosefu mkubwa wa maji unaoendelea kulikumba eneo la pembe ya Afrika na kuwaathiri mamilioni ya watu nchini Somalia , Ethiopia na Kenya. Mpongo huo unaofadhiliwa na serikali ya Japan kwa kima cha dola milinoni 1.55 utang’oa nanga kupitia kuendeshwa utafiti wa uwezekano wa kupatikana kwa amji kwenye sehemu zilizoathiriwa na ukame. Joseph Massaquoi ni mkurugenzi wa UNESCO ofisi ya Nairobi.

(SAUTI YA JOSEPH MASSAQUOI)