Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa ombi la fedha kuwasaidia waliokimbia makwao nchini Mali

IOM yatoa ombi la fedha kuwasaidia waliokimbia makwao nchini Mali

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la dharura la dola milioni 3.5 zitakazofadhili shughuli za kutoa usaidizi kwa raia wa Mali ambao wamekimbia mapigano kaskazini mwa nchi na kutafuta makao kwenye mji mkuu Bamako pamoja na miji ya Mopti na Kayes.

IOM inashirikiana na wapatanishi wengine likiwemo shirika la msalaba mwekundu nchini Mali ili kuweza kuwafikia wakimbzii wa ndani ambao wamekwama kwenye sehemu zinazokumbwa na mapigano za kaskazini mwa nchi. Ufadhili huo pia unahitajika kuzipa msaada familia ambazo zimewapa makao waliohama makwao ambazo kwa sasa zimeathiriwa na ukame na ambazo hazina uwezo wa kuwahudumia watu wanaondelea kuwasili mwenye sehemu hizo.

IOM ina hofu kwamba ukosefu wa usaidizi ndani mwa Mali ni ambalo litawalazimu wakimbizi zadi wa ndani kuhamia mataifa jirani kama Mauritania, Burkina Faso na Niger.Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Nalo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Linasema kuwa hali iliyo sasa kaskazini mwa Mali inahatarisha afya ya akina mama na watoto ambapo zaidi ya watoto 560,000 wannasumbuliwa na utapiamlo.