Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yazidi kuwa mbaya katika eneo la Sahel:WFP,UNHCR

Hali yazidi kuwa mbaya katika eneo la Sahel:WFP,UNHCR

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR wamezindua oparesheni ya dharura kwa maelfu ya watu ambao wamekimbia makwao kufuatia mzozo unaondelea nchini Mali na ambao kwa sasa wamevuka mpaka na kuingia mataifa jirani.

Mkurugenzi wa WFP Ertharin Cousin anasema kuwa wanaendelea kushirikiana na UNHCR kusaidia familia zilizolazimishwa kuhama makwao nchini Mali na ambazo kwa sasa zinahitaji misaada ya dharura ya chakula na makao.George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)