Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya raia wa DRC wakimbilia Uganda

Maelfu ya raia wa DRC wakimbilia Uganda

Karibu watu 15,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamekimbilia Kusini Magharibi mwa Uganda wakati kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kati ya vikosi vya DRC na makundi ya waasi.

Wafanyikazi kutoka shirika la kuhudumia wakimbzi la Umoja wa Mataifa UNHCR wanasema kuwa watu 7000 kati ya waliolazimika kuhama makwao wamepiga kambi kwenye mji wa Bunagana huku wengi wao wakiwa wanatokea vijiji vilivyo Kivu Kaskazini huku takriban watu 9,000 wakiwa wamevuka mpaka na kuingia Rwanda.

Andrej mahecic kutoka UNHCR anasema kuwa jitihada zinafanywa kuwasafirisha watu hao kwenda maeneo salama mbali na mipaka.

(SAUTI YA ANDREA MAHECIC)