Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia uko katika kipindi kigumu na muhimu:Al-Nasser

Uchumi wa dunia uko katika kipindi kigumu na muhimu:Al-Nasser

Uchumi wa dunia umeelezwa kuwa katika kipindi kigumu na muhimu sana. Hayo yamesemwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser akifungua mjadala wa ngazi ya juu kuhusu hali ya uchumi duniani, fedha na athari zake kwa maendeleo mwaka 2012.

Bwana Al-Nasser amesema karibu kila siku tunatambua kwamba kuna shinikizo za kiuchumi na kifedha ambazo zinahitaji kushughulikiwa, endapo dunia inataka kufufua, kukuzana kujumuisha wote katika ufufuaji wa uchumi. Ufufuaji ambao utachagiza maendeleo, kuimarisha hali ya ajira, na kuwatoa mabilioni ya watu katika umasikini.

Ameongeza kuwa inajulikana bayana, kwamba mdororo wa uchumi umeathiri nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea.

(SAUTI YA AL-NASSER)