Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo mpya unahitajika kwa ajili ya mabadiliko ya ukuaji wa Uchumi:Ban

Mfumo mpya unahitajika kwa ajili ya mabadiliko ya ukuaji wa Uchumi:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mfumo wa zamani wa ukuaji uchumi umesambaratika na hivyo mfumo mpya unahitajika kwa ajili ya mabadiliko ya ukuaji. Akizungumza Alhamisi katika mjadala wa ngazi ya juu kuhusu “hali ya uchumi wa dunia na fedha na athari zake katika maendeleo” Ban amesema ukuaji unaotakiwa ni ule ambao ni wa usawa, ukuaji ambao utaendelea katika mipaka tuliyonayo ambao utawafaidi kizazi cha sasa na kijacho.

Ban ameongeza kuwa huu ndio utakuwa mtazamo kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu mwezi ujao mjini Rio de Janeiro Brazili kwenye Rio+20. Amesema hiyo itakuwa fursa muhimu ya kuanzisha mfumo mpya unaozingatia yanayowezekana na kuacha yasiyowezekana kwani kinachohitajika ni mapinduzi ya mtazamo wa chanzo cha ukuaji uchumi, kupatikana ajira na fursa kwa wote.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)