Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa Kiasili wanahitaji Usaidizi wa Kifedha na Kitaaluma

Watu wa Kiasili wanahitaji Usaidizi wa Kifedha na Kitaaluma

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Nassir Abdulaziz Al-Nasser, amesema kuwa watu wa kiasili wanahitaji usaidizi wa kifedha na kitaaluma, ili kuwezesha kuzilinda haki zao. Bwana Al-Nasser ameyasema hayo leo kwenye hafla ya kuadhimisha miaka mitano tangu kutangazwa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa kiasili. Abdulaziz Al-Nasser ametoa wito kwa serikali kote duniani kuchangia fedha zinazosaidia kuendeleza haki za watu wa asili. Amesema, tayari kuna baadhi ya njia zinazowezesha usaidizi huu kufanywa.

(SAUTI YA AL-NASSER)

Baadhi ya hizi ni Hazina ya Kujitolea ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Watu wa Kiasili, na Hazina ya Mwongo wa Pili wa Watu wa Kiasili, pamoja na Hazina nyingine za mashirika ya Umoja wa Mataifa. Baraza Kuu limehimiza serikali, mashirika baina ya serikali na yale yaso ya kiserikali, taasisi za kibinafsi na hata watu binafsi, kuendelea kuchangia hazina hizi. Ninaongeza sauti yangu kwa wito huu.