Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yafanya mabadiliko kwenye mawasilino ya mtandao

ITU yafanya mabadiliko kwenye mawasilino ya mtandao

Chama cha kimataifa cha mawasiliano ITU kimetoa ripoti yake ya mwaka 2012 kuhusu mabadiliko kwenye mawasiliano ambayo inaonyesha umuhimu wa kubuniwa kwa vifaa vipya vya kiteknolojia na huduma.

Kwa muda wa miaka mitano iliyopita watumizi wa mtandao kupitia kwa simu wameongezeka hadi watu milioni 591 mwaka huu ambapo asilimia kubwa wako kwnye mataifa yaliyoendelea huku gharama inatajwa kuwa kizuizi kikubwa hasa barani Afrika.

Kutokana na makadirio ya ITU ni kwamba idadi ya watu wanaotumia mtandao wa simu duniani imepita watu bilioni moja huku asimilia 8.5 ya watu kutoka nchi zinazoendea ikiwa ndiyo inayotumia mtanadao wa simu. Sanjay Acharya ni msemaji wa ITU.