Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utazamaji wa ndege utachangia kuboreka kwa sekta ya utalii:UNEP

Utazamaji wa ndege utachangia kuboreka kwa sekta ya utalii:UNEP

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limesema kuwa utazamaji wa ndege ni kivutio kikubwa cha utalii ambacho kinaweza kuwa chenye manufaa kwa uchumi liongeza kuwa mataifa yanastahili kufanya jitihada za kuinua sekta hii inayoendelea kukua.

Kaimu katibu kwenye makubaliano ya kulinda ndege wahaohama Elizabeth Maruma Mrema amesema kuwa utazamaji wa ndege unachangia pakubwa kwenye ukuaji wa sekta ya utalii na una manufaa ya moja kwa moja kwa nchi nyingi.

Siku ya utazamaji wa ndege dunaini ambayo inaadhimishwa kati ya tarehe 12-13 mwezi huu ina lengo la kuonyesha manufaa haya na kutoa hamasisho, kuhusu umuhimu wa kulinda ndege.