Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Valerie Amos atoa wito kwa jamii ya Kimataifa kuendelea kuwasaidia raia wa Afghanistan

Valerie Amos atoa wito kwa jamii ya Kimataifa kuendelea kuwasaidia raia wa Afghanistan

Mratibu Mkuu wa Huduma za Kibinadamu na Mipango ya Dharura wa Umoja wa Mataifa, Bi Valerie Amos, ametoa wito kwa wafadhili kuendelea kuwasaidia raia wa Afghanistan, wakati akizuru taifa hilo kwa mara ya kwanza.

Bi Amos anazuru Afghanistan kukagua hali ya kibinadamu nchini humo, na wakati akiwa huko, atakutana na wawakilishi wa serikali na washirika wengine, ili kujadili hali hiyo ilivyo.

Baada ya kukutana na Makamu wa rais, Mohammad Karim Khalil, Bi Amos amesema kuwa mashirika ya kutoa misaada yamekuwa nchini Afghanistan kwa karne nyingi, na yataendelea kuwasaidia watu wa Afghanistan wakati wa mabadiliko na hata baadaye. Amesisitiza kuwa kipindi cha mabadiliko kitahitaji usimamizi makini.