Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umejidhatiti kuzisaidia nchi zilizokumbwa na vita kujenga upya amani:Ban

UM umejidhatiti kuzisaidia nchi zilizokumbwa na vita kujenga upya amani:Ban

Umoja wa Mataifa umejidhatiti kufanya kila liwezekanalo kuzisaidia jamii zilizosambaratishwa na vita ili zisirejee tena katika mkondo huo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipozungumza na umati wa watu kwenye makao makuu ya Marekani Washington hii leo.

Ban ameongeza kuwa wakati kumekuwa na vikwazo kadhaa ujenzi wa amani unasalia kuwa kiuungo muhimu katika juhudi za Umoja wa Mataifa.

Katika hotuba yake kwenye kituo cha masuala ya kimataifa Washington D.C, Ban ameainisha majukumu ya mipango 16 ya operesheni za amani za Umoja wa Mataifa na mipango 15 inayohusika na masauala ya ujenzi wa amani jambo alilosema ni kitovu cha majukumu ya Umoja wa Mataifa.

Ban amesisitiza kwamba ujenzi wa amani unaokoa maisha , kulinda haki za binadamu na kuchagiza utawala wa sheria, akiongeza kwamba pia unaokoa fedha, kwa gharama zinazosababishwa na operesheni za kijeshi na athari za kichumi zinazosababishwa na vita.