Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la watu wa asili kuadhimisha mwaka wa tano wa haki zao laanza New York

Kongamano la watu wa asili kuadhimisha mwaka wa tano wa haki zao laanza New York

Kongamano la kimataifa la watu wa asili lililoitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon limeanza Jumatatu kuadhimisha mwaka wa tano tangu kupitishwa kwa azimio la kulinda haki za watu wa asili.

Kongamano hilo la wiki mbili likihusisha mikutano kadha wa kadha linafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwenye ukumbi wa Baraza Kuu.

Kongamano hilo pia litatathimini jukumu la azimio lililopitishwa katika kutimiza wajibu wa kulinda haki za watu wa asili duniani. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)