Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikakati ya usalama kwa waandishi wa habari yapitishwa na UM

Mikakati ya usalama kwa waandishi wa habari yapitishwa na UM

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua kuhusu usalama wa waandishi wa habari na masuala ya ukatili, wakiongozwa na shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO na bodi ya wakurugenzi wa Umoja wa Mataifa wameidhinisha hapo April 13 mwaka huu njia za ushirikiano katika mfumo wa Umoja wa Mataifa ambazo zitalinda usalama wa waandishi wa habari.

Mpango huo wa kuchukua hatua una lengo la kuanzisha mazingira huru na salama kwa waandishi habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari katika maeneo yenye migogoro na yasiyo na vita, kwa mtazamo wa kuimarisha amani, demokrasia na maendeleo kote duniani.

Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema uhuru wa waandishi wa habari ni muhimu katika utekelezaji wa kifungu namba 19 cha azimio la haki za binadamu ambalo linasisitiza haki ya uhuru wa kujieleza. David Okwemba ni muandishi habari na mhariri Afrika ya Mashariki.

(SATI YA DAVID OKWEMBAH)