Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

UM waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

Uhuru wa kujieleza ni moja ya haki muhimu kwa watu, na ni uhuru unaozidi uhuru wa aina yoyote ile na kutoa msingi wa utu wa mtu. Haya yameelezwa katika taarifa ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova.

Taarifa yao ikitoa ujumbe maalumu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari imesema , vyombo vya habari huru, vinavyojumuisha wote na vinavyojitegemea ni muhimu katika kufanikisha azimio hii.

Irina Bokova amesema uhuru wa vyombo vya habari unatoa matumaini ya kuleta mabadiliko katika jamii kupitia masuala ya uwazi na uwajibikaji, na siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni fursa nzuri ya kuelimisha kuhusu vita vya kuhakikisha hatua zinapigwa katika kupatikana kwa uhuru huo.

(SAUTI YA IRINA BOKOVA)

Nao wananchi kutoka Afrika ya Mashariki wana maoni gani kuhusu suala hili na siku ya uhuru wa vyombo vya habari?

(MAONI AFRIKA MASHARIKI)