Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan na Sudan Kusini kukabiliwa na vikwazo endapo mapigano hayatokoma

Sudan na Sudan Kusini kukabiliwa na vikwazo endapo mapigano hayatokoma

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio Jumatano linalozitishia Sudan na Sudan Kusini na uwezekano wa kukabiliwa na vikwazo endapo hawatokomesha machafuko yanayoendelea.

Nchi hizo mbili jirani zimekuwa zikipigania mafuta, mpaka na masuala ya uraia. Azimio la leo linasisitiza haja ya kurejesha mara moja amani ya kudumu. Na kama upande wowote utashindwa basi Baraza la Usalama litachukua hatua ambazo sio za kijeshi ikiwemo vikwazo vya kiuchumi.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema azimio hilo linadhihirisha nia ya pamoja ya baraza ya kusaidia mpango wa amani wa muungano wa Afrika.