Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibikaji ni bora kuliko kutojali ukatili dhidi ya wanawake:Manjoo

Uwajibikaji ni bora kuliko kutojali ukatili dhidi ya wanawake:Manjoo

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Rashida Manjoo ameitaka serikali ya Papua New Guinea kutumia sheria na kutoa msaada wa kiufundi katika mapambano ya kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.

Akihitimisha ziara yake ya kwanza nchini humo Bi Manjoo ameutaka pia uongozi wa taifa hilo kushughulikia baadhi ya mila na tamaduni ambazo zinawakandamiza wanawake. Manjoo amesema uwajibikaji zaidi badala ya kutojali iwe ndio mfumo kwa vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake.

(SAUTI YA RASHIDA MANJOO)