Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova ataka kutumika kwa sayansi kuinua maisha ya watu

Bokova ataka kutumika kwa sayansi kuinua maisha ya watu

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa Irina Bokova ametaka kuwe na ushirikaino kati ya masuala ya Sayansi na Sera na kutoa mwelekeo wa umuhimu wa utafiti wa kisayansi katika maendeleo.

Bokova aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mawaziri mjini Nairobi Kenya ambalo ndilo kongamano la kwanza  kuhusu sayansi , teknolojia na uvumbuzi kuandaliwa barani Afrika.

Mkutano huo ulifunguliwa na rais wa Kenya rais Mwai Kibaki na kuhudhuriwa na rais wa benki ya maendeleo barani Afrika Donald Kaberuka pamoja na makamu wa rais kwenye tume ya muungano wa Afrika Erasmus Mwencha. 

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)