Ban ataka hatua kuchukuliwa dhidi ya wasafirishaji haramu wa watu

3 Aprili 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa wanaosafirisha watu kiharamu hawastahili kupewa nafasi kwenye ulimwengu huu. Kwenye taarifa yake iliyowasilishwa kwenye mkutano kuhusu vita dhidhi ya usafirishaji haramu wa watu uliondaliwa mjini New York Ban alitoa wito kwa serikali zote kupambana na vitendo vya usafirishaji haramu wa watu kuambatana na haki za kimataifa za binadamu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Mkutano huo ulihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa na wataalamu wa kupambana na usafirishaji haramu wa watu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud