Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lasikitishwa kuhusu ushirikiano wa kisiasa nchini Yemen

Baraza la Usalama lasikitishwa kuhusu ushirikiano wa kisiasa nchini Yemen

Viongozi wa kisiasa nchini Yemen wametolewa wito wa kuwa na dhamira katika kipindi cha mpito na kuchukua jukumu katika ujenzi wa mchakato huu.

Wito huu umetolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika taarifa iliyoelezea wasiwasi kuhusu kuzorota kwa ushirikiano kutokana na uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni.

Balozi wa Uingereza Mark Lyall Grant ndiye rais wa Baraza la Usalama wa mwezi machi.

(SAUTI YA MARK LYALL GRANT)

Mwezi wa Februari watu wa Yemen walipiga kura ya kuchagua rais mpya baada ya zaidi ya miongo mitatu ya utawala wa rais Ali Abdullah Saleh.

Kura hii ilikuwa moja ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana baada ya miezi ya maandamano.